Tuesday, 8 November 2011
RAIS NA UGENI TOA UK
Rais Jakaya Kikwete akiwa katika dhifa ya taifa aliyomuandalia mwana wa Malkia wa Uingereza, Prince Charles ambaye anatarajiwa kumaliza ziara yake ya siku tatu leo.
Tuesday, 1 November 2011
JENGO LA QUALITY CENTRE LINA MENGI
| Jengo la Qality Centre |
Na Mwandishi Wetu
Kama hujatembelea jengo jipya la biashara la Qality Centre lililopo Barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, basi tembelea leo kwani unapitwa na mambo mengi.
Nilibahatika kutembelea jengo hilo na nikashuhudia mambo mengi ya kuvutia. Kwanza, ni kwamba kila kitu unaweza kukipata ndani ya jingo hilo, iwe chakula, michezo kwa watoto wao hata watu wazima na bidhaa mbalimbali kwa kuwa kuna maduka ya ‘nguvu yaani Mall.
Ndani ya jengo hilo kuna benki nne ambazo zitakuwa na kazi ya kuhudumia wateja mbalimbali bila ubaguzi. Kwa mujibu wa Meneja wa Maendeleo ya Biashara wa jingo hilo, Sarah Pima, nia ya kukusanya shughuli zote ndani ya mjengo huo ni kuwaondolewa usumbufu wateja.
“Tumefanya hivi ili mteja anapokuja hapa apate kila kitu humu, chakula, vifaa mbalimbali vya stationary, nguo na hata burudani kwao na watoto wao,” alisema Sarah.
Nilipotembelea jengo hilo la ghorofa nilishuhudia ngazi zinazotumia umeme, na maduka yenye nguo nadhifu pamoja na duka kubwa sana la Supermarket ambalo lipo juu na chini kwakuwa ni ghorofa.
Kuna Amazon Pub na Savannah Lounge ambapo wateja watakuwa na nafasi ya kuburudika na chochote watakachopata lakini pia kuna screen mbili kubwa za runinga, hivyo mteja anaweza akawa anakunywa kinywaji akipendacho huku akifuatilia mambo mbalimbali katika runinga.
WATOTO
Qality Centre haikuwasahau watoto, imewajengea sehemu maalum ya kuchezwa. Kuna michezo mingi kama vile magari, helikopta, pikipiki na hata michezo ya kudungua kwa kutumia bunduki bandia. Lakini kuna jingo la majini ambalo wenyewe kwa mujibu wa Meneja Sarah linaitwa Horrow House.
Nilitembelea jingo hilo nikakutana na ubunifu wa hali ya juu. Ndani kuna majini ambayo yanatisha. Wapo waliosimama, aliyekaa, waliofungiwa vyumbani na kuna ‘mait’ inayonyanyuka na kupiga kelele za kutisha. Yupo ‘jini’ la kike ambalo licha ya kuwepo kwa kitanga, halitulii, linapiga kelele huku likielea angani. Ni mambo ya kutisha. Kuna vyumba vine vya sinema. Meneja Sarah anasema kila sinema zitakuwa zikioneshwa na uzinduzi utafanyika Novemba 4 mwaka huu. Nisimalize uhondo, nenda katembelee leo, utaburudika na kushangaa mengi.
Subscribe to:
Comments (Atom)